MWENYEKITI wa Klabu ya
Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amekataa katakata kuwataja
wanachama wanaodaiwa ni mashoga ndani ya klabu hiyo ya jijini Dar.
Akizungumza na Amani juzikati jijini Dar baada ya kuombwa kuwataja
wadaiwa hao, Steve alisema hashindwi kuyaanika majina yao, bali uongozi
wake kwenye chama hicho si kuingilia mambo binafsi bali kuunganisha
umoja na mshikamano kwa ajili ya tasnia ya filamu za Bongo.
“Hilo suala kila mtu ananiachia mimi nilizungumzie kwa
kukanusha au kuweka majina hadharani ya wanaodaiwa ni mashoga. Hadi
namaliza uongozi wangu sitafanya hivyo,” alisema Steve.
Pichani ni baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi.
Siku za hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari viliwahi kuripoti
suala la kuwepo kwa mastaa mashoga kwenye klabu hiyo yenye nguvu ya
ushawishi wa fedha mjini.

0 Comments