Unakumbuka kipindi Wema Sepetu amenyoa kipara na kupiga picha na mchumba
wake Diamond Platnumz zilizopata comments na likes nyingi Instagram?
Alinyoa kipara kuigiza kama mgonjwa wa saratani kwenye filamu yake mpya
iitwayo Family aliyoshirikiana na Aunty Ezekiel.
Kwa mujibu wa tovuti ya Bongo5, Family ni filamu tofauti na zile za kibongo
ulizozizoea kuziona.
''Mimi naimani kuwa tasnia ya bongo movie watu
walishazoea mfumo mmoja, story za aina moja, story zetu most of the time
mimi huwa naziita story za kwenye makochi na za juice,'' alisema.
''Kwasababu unaweza ukashangaa mtu amekaa kwenye kochi yaani yeye story
imeenda imerudi wako kwenye makochi tu sebuleni, wamehama sana wameenda
chumbani, hawathink out of the box. Na story ziko zilezile, mke sijui
hawezi kuzaa, kuna sijui uganga. Sisi tumefanya kwanza research,
tukaangalia story ambayo iko different, story ambayo hawajafanya watu
wengi.
Tumehit target nyingine, it's about cancer, kwenye hiyo story ni
mgonjwa wa cancer na ndio maana kuna kipindi mliniona nimenyoa kabisa
kipara.
Watu wengi walijiuliza kwanini Wema kanyoa lakini the aim was
kudeliver kile kitu ambacho nilitaka kudeliver kuwe kuna uhalisia


0 Comments