Kiungo wa Manchester
City Yaya Toure, 31, amekataa kujiunga na Manchester United (Daily
Star), kiungo wa Everton Ross Barkley, 20, anatazamwa na Man City kuziba
nafasi ya Yaya Toure, iwapo atalazimisha uhamisho na kuondoka
Etihad (Daily Mail), beki wa kulia wa Arsenal Carl Jenkinson, 22,
anasakwa na West Ham (Sun), Sunderland wamemuulizia winga wa Atletico
Madrid Cristian Rodriguez, 28, (Daily Mail) mshambuliaji wa zamani wa
Man City Mario Balotelli, 23, ameonesha dalili kubwa za kutaka kuhamia
Arsenal, baada ya kupiga picha mbele ya nembo ya Arsenal (Daily Star),
meneja wa Liverpool Brendan Rodgers anataka kuendelea kununua wachezaji
licha ya matumizi ya Liverpool kuonekana huenda yakazidi pauni milioni
100, kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo (Liverpool Echo),
Liverpool imeulizia kama wanaweza kumchukua winga wa PSV Eindhoven
Zakaria Bakkali (Daily Express), Kiungo wa Real Madrid Sami Khedira
anafikiria kuzikataa Arsenal na Chelsea na kusalia na mabingwa wa Ulaya
(Daily Express), boss wa West Brom Alan Irvine amesema hatua ya
Manchester United kumnunua Luke Shaw kwa pauni milioni 30 imesababisha
bei ya mabeki kupanda (Daily Mirror), meneja mpya wa Manchester United
Louis van Gaal anataka kumteua Paul Scholes kuwa mmoja wa wasaidizi wake
(Manchester Evening News), Van Gaal pia ametaka uwanja wa mazoezi wa
Carrington kufanyiwa mabadiliko kwa sasaba "una upepo mkali" (Daily
Mail), kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere amerejea mapema na kuanza
mazoezi baada ya kushutumiwa kwa kuonekana akivuta sigara mjini Las
Vegas (Daily Telegraph), na hatimaye winga kutoka Ufaransa Hatem Ben
Arfa ameingia katika mzozo na klabu yake ya Newcastle kuhusiana na
"unene" wake, yeye anadai amejenga misuli na kusema ni makosa kwa
Newcastle kumpiga faini kwa kudai ni "manyama uzembe" (Daily Mirror).
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
0 Comments