
STAA wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bela’ na mpenzi
wake wa kitambo, Karama Omari ‘Luten’ wanatarajia kufunga ndoa Novemba,
mwaka huu.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Isabela
ambaye anatamba na wimbo wa Taratibu alisema ana furaha isiyo na kifani
kwani kwa mara ya kwanza tangu aanze uhusiano wa kimapenzi na Karama
amemtamkia suala la ndoa.
Msanii wa Bongo Fleva Karama Omari ‘Luten’ .
“Yaani nina furaha sana kwani Karama hakuwahi kunitamkia kwamba
atanioa lakini hivi karibuni ametamka tena mbele za watu naamini ndoa
yetu itakuwa ya baraka kwani mama Rolaa amejitolea kutufanyia sherehe
ambapo ameahidi kutoa milioni tano, bado marafiki zake,” alisema Bela.
0 Comments