Kijana
mmoja aliyejulikana kwa jina la Vicent Kawawa(28) ameuawa kwa kupigwa
na fimbo na kitu kizito kichwani na mganga wa kienyeji aliyekuwa
anamtibu ugonjwa wa akili nyumbani kwake katika kijiji cha Buduba kata
ya Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha
alisema tukio hilo limetokea Agosti 5 mwaka huu saa 12 jioni.
Alisema Vicent Kawawa(28) mkazi wa kijiji cha Buduba akiwa nyumbani
kwa mganga wa jadi aitwaye Mihayo Isheli akitibiwa ugonjwa wa akili
aliuawa kwa kupigwa na fimbo na kitu kizito kichwani na mganga huyo na
watu waliokuwepo eneo la tukio na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kamanda Kamugisha alisema chanzo cha tukio hilo ni kwamba mgonjwa
alipandisha kichaa na kuanza kumpiga mganga wa jadi na watu waliokuwa
eneo hilona ndipo katika kumtuliza mganga alianza kumpiga akisaidiwa na
watu hao ambao idadi yao haijajulikani na kusababisha kifo chake papo
hapo.
Alisema baada ya tukio hilo mganga Mihayo Isheli alikimbia na familia
yake pamoja na watu waliokuwa katika eneo hilo na kamba jeshi la polisi
linaendelea na uchunguzi sambamba na kumtafuta mganga huyo wahusika
wengine waliokuwa katika eneo la tukio.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
0 Comments