
Siku
mbili zilizopita kumekuwa na taarifa mitaani kuwa mwimbaji ambaye pia
ni producer wa Sharobaro Records, Bob Junior alifanyiwa fujo na mwanaume
mmoja anaedaiwa kuwa mume wa msichana aliyekuwa anafanya naye video.
Taarifa
hizo zilieleza kuwa tukio hilo lilifanyika maeneo ya Mlimani City
wakati Bob Junior alipokuwa akishuti vipande vya wimbo wake wa ‘Bolingo’
huku msichana huyo akijiachia mbele ya lens.
Ghafla
mumewe akatokea na kuzua tafrani, video ya wimbo ikageuka kuwa ya
ndondi na mwisho wa siku mwimbaji huyo alilazimika kukimbia kupisha
shari.
Times Fm imeongea na Bob Junior kuhusu tetesi hizo ambapo yeye amekiri
kutokea kwa fujo hiyo lakini amekanusha kuhusu suala la kufanya video
na msichana huyo ingawa alikuwa na directors wake na vifaa.
“Hapana,
naona watu wanakuwa kama wambea. Mimi nilikuwa nimekaa pale Mlimani
City tunapiga story niko na mwanamke wangu. Rafiki yangu mwingine
alikuwa kakaa na mwanamke mwingine, sasa sijui kama ni mke wa mtu au
nini, ndio ikatokea vurugu lakini huyo mwanamke aliyefanyiwa vurugu mimi
simfahamu.” Ameeleza Bob Junior.
“Tulikuwa
tumekaa tu tunaenjoy tunapiga story, tunakula…mimi sijui kama ni
mwanamke wake au ni mke wake. Amemfanyia vurugu, amemvuta nywele.
Wamezinguana kidogo lakini sifahamu kama ni mke wake au ni mchumba wake
ila najua ni mtu ambaye ana uhusiano nae.” Ameongeza.
Akizungumzia
kuhusu taarifa kuwa alitoka nduki na kumuacha rafiki yake akifanyiwa
fujo, Bob ameeleza kuwa aliondoka kupisha shari na sio kukimbia kama
ilivyotafsiriwa.
“Hapana
siwezi kukimbia siwezi kukimbia. Tanzania ni nchi yenye amani kwa nini
nikimbie kuna vita gani jamani hapo. Mimi nilichukua vitu vyangu na
vijana wangu na team Sharobaro wangu, nikaondoka taratibu nikachukua
gari langu nikaondoka. Unapoona mtafaruku hupaswi kukaa kuendelea
kuangalia jambo. Unapaswa kupisha uliache jambo liendelee.”
0 Comments