Chama
cha Mapinduzi -CCM kimedai kuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya
katiba Jaji Joseph Warioba na baadhi ya wajumbe wa tume yake
wamemshambulia kwa maneno Mwenyekiti wa chama hicho rais Jakaya
Kikwete
Hatua
hiyo imefikiwa kutokana na Mdahalo ulioandaliwa na taasisi ya mwalimu
Nyerere ambao umefanyika Jumatatu wiki hii na kwamba kupitia mdahalo huo
Jaji Warioba na wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba waliitupia
lawama CCM na mwenyekiti wake kwamba hoja zake ni nyepesi, dhaifu na za
kutunga.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya taifa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye
amesema Jaji Warioba na tume yake wameugeuza mchakato wa katiba kama
mradi wao binafsi hali inayosababisha wasikubaliane na mtu yeyote
anayetaka kutofautiana nao kimawazo
Nape Amewataka waache kuchafua mchakato wa katiba unaoendelea bungeni mjini Dododma
Aidha
Nape amesema wanayo haki ya kutoa maoni yao kama wanavyoona kwao
inafaa kwa kuzingatia katiba ya CCM, Sera na Ilani ya chama hicho.
0 Comments