MWANAMAMA Corinne Diacre
anayeinoa klabu ya Clermont Foot ya Ufaransa amepoteza mchezo wake wa
kwanza akiwa kocha wa timu hiyo kwa kufungwa mabao 2-1 na timu ya
Brest. Mechi hiyo ya Ligi Daraja la Pili nchini Ufaransa ilishuhudia kwa
mara ya kwanza mwanamke akiisimamia timu ya wanaume kama kocha katika
ligi ya Ulaya. Clermont ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza
kupitia kwa Souleymane Sawadogo katika kipindi cha kwanza kabla ya
wapinzania kufunga mabao mawili na kuibuka washindi katika kipindi cha
pili. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Diacre amesema kufungwa siku
zote sio jambo zuri lakini hana chaka kwamba timu yake itafanya vyema
msimu huu. Kocha alisherekea miaka 40 ya kuzaliwa kwake jana na alipokea
shahada la maua na busu katika shavu kutoka kwa kocha mwenzake wa timu
pinzani ya Brest, Alex Dupont kabla ya kuanza kwa mchezo huo. Diacre
alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo Juni mwaka huu akichukua nafasi ya
mwanamke mwenzake Helena Costa ambaye alijiuzulu kabla ya kucheza mechi
hata moja akiituhumu Clermont kwa kushindwa kumheshimu.
0 Comments