NYOTA wa klabu ya
Barcelona Neymar na Lionel Messi wamerejea mazoezini leo baada ya likizo
ndefu ya Kombe la Dunia wakiwa sambamba na Javier Mascherano na Dani
Alves. Hatua ya fainali iliyofikiwa na Argentina katika michuano hiyo
imesaidiwa kwa kiasi kikubwa na Messi na Mascherano wakati Alves alikuwa
sehemu ya kikosi cha Brazil kilichimaliza katika nafasi ya nne na sasa
kocha mpya Luis Enrique anaweza kuwajumuisha wachezaji hao katika
maandalizi ya msimu mpya. Neymar ambaye aliumia mgongo katika mchezo war
obo fainali dhidi ya Colombia yeye amerejea lakini hataweza kujiunga na
wenzake wakati akiendelea kupona badala yake atakuwa akifanya mazoezi
peke yake. Mechi za kirafiki za Barcelona walizocheza mpaka sasa
zimekuwa za kusuasua ambapo wameambulia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Recreativo Huelva na sare ya bao 1-1 baada ya wiki tatu za mazoezi. Hata
hivyo bado wanakabiliwa na mechi zingine za kujipima nguvu dhidi ya
Napoli, HJK na Leon kabla ya kucheza mechi yao ya ufunguzi wa La Liga
dhidi ya Elche Agosti 24 mwaka huu.
0 Comments