Advertisement

Responsive Advertisement

Mashoga na Wasagaji Sasa Kupigwa Mawe Hadharani Nchini Kenya


Ripota toka   nchini Kenya Julius Kipkoech anaripoti kwamba nchi hiyo inarejea kwenye headlines kuhusu maswala ya kubuni sheria za kipekee ambapo sasa bunge la kitaifa linapanga kujadili sheria inayopendekezwa kwamba raia yeyote wa kigeni anayepatikana akishiriki uhusiano wa jinsia moja ahukumiwe kupigwa mawe hadharani hadi kufa na kama ni raia wa Kenya basi ahukumiwe kifungo cha maisha jela.

Mwandishi na mdhamini wa sheria hiyo Edward Onwong’a Nyakeriga anapendekeza kuharamishwa kwa ulawiti na kuhukumiwa jela kwa wanaotenda kosa hilo huku akisisitiza” “Upo umuhimu wa kuwalinda watoto na vijana ambao wanalengwa na dhulma ambazo kwa mda mrefu zinaepukwa kutokana na mabadiliko, teknolojia na habari isiyo chujwa na watoto mayatima kukosa mwakilishi pamoja na majaribio ya wanaoshiriki uhusiano wa jinsia moja kuwalea watoto ilihali wanaendeleza uhusiano wao”

Mswada huu wa chama cha Republican Liberty Party unaharamisha uhusiano wowote wa jinsia moja na tayari spika wa Bunge la kitaifa Kenya Justin Muturi ameupokea na kuuwasilisha kwa kamati ya sheria bungeni ambayo inatathmini kisha kutoa ripoti kwa bunge.
Bonyeza Like Kama Story imekuvutia:
BOFYA HAPA LIKE PAGE YETU ILI UWE WA KWANZA KUPATA HABARI ZETU KEMKEM ..