SHIRIKISHO la Soka
Tanzania-TFF limeiteua klabu ya Azam kuiwakilisha Tanzania Bara katika
michuano hiyo baada ya waandaaji wake, Baraza la Vyama vya Mpira wa
Miguu Afrika Mashariki na Kati-CECAFA kuamua kuindoa Yanga iliyokuwa
icheze awali. CECAFA imesema baada ya majadiliano na Yanga kupitia TFF,
klabu hiyo ilipewa muda hadi jana iwe imetekeleza matakwa ya kikanuni
ili iruhusiwe kushiriki michuano hiyo lakini haikufanya hivyo. Yanga
iliwasilisha orodha ya wachezaji wengi wa kikosi cha pili kwa ajili ya
kushiriki michuano hiyo, jambo ambalo limekatawaliwa na CECAFA kwa vile
linakwenda kinyume na kanuni za michuano hiyo. Azam FC ambayo ilishika
nafasi ya pili- nyuma ya Yanga katika ligi iliyopita msimu wa 2012/2013
imekubali kushiriki michuano hiyo na inatarajia kuondoka nchini kesho
kwenda Kigali. Msafara wa Azam FC katika michuano hiyo unaongozwa na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, James Mhagama.
0 Comments