Malunde1 blog imefuatilia kwa ukaribu
zaidi kuhusu ajali ya Basi iliyotokea usiku huu saa 4,ambapo tumeelezwa
kuwa basi lililopata ajali ni basi la Musoma Express lenye namba za
usajili T138 BDQ lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Musoma.
Basi hilo limepata ajali katika eneo la Usanda hatua chache baada ya kutoka katika mzani wa Tinde barabara ya Tinde Shinyanga.
Inaelezwa kuwa wakati dereva akiendesha basi hilo ghafla mwanamme mmoja anayedaiwa kuwa ni mzee (mtembea kwa miguu) alikatisha barabarani na kusababisha ajali hiyo.
Jeshi la polisi limefika katika eneo la ajali.
Malunde1 blog imezungumza na mmoja wa askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga aliyeko katika eneo la tukio,ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu yeye siyo msemaji, amesema mwanamme aliyegongwa na gari hilo amefariki dunia papo hapo na kwamba abiria waliokuwa kwenye basi hilo wako salama(hakuna majeruhi wala waliopoteza maisha).

0 Comments