Mwaka 2013 ni watu wachache tu
waliokuwa wakilifahamu jina la Nuh Mziwanda kwakuwa alikuwa msanii
mchanga anayetafuta nafasi yake kwenye muziki wa Tanzania. Wimbo wake
ulioanza kumtambulisha uliitwa ‘Otea Nani’ ambao ulipata nafasi kiasi
kwenye vituo vya redio. Lakini jina la muimbaji huyo
lilikuja kuwa kubwa zaidi baada ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na
Shilole, uhusiano ambao umekuwa wa wazi katika mitandao yao ya kijamii.
Kuonesha kuwa ana mapenzi ya kweli kwa Shilole ambaye ni mama wa watoto
wawili, Nuh alijichora tattoo mkononi yenye jina la Shilole. Shilole pia aliamua kumpa shavu
mpenzi wake kwa kuonekana kwenye video ya wimbo wake ‘Msondongoma’ na
hivyo kumwongezea wigo zaidi. “Yeye ndo Mama watoto Mungu akijaalia,”
aliandika Nuh kwenye picha ya Shilole aliyoiweka kwenye akaunti yake
mtandao wa Instagram yenye followers zaidi ya 19,000. “Ukichagua kitu roho yako
inapenda raha sana.sasa kwa mfano mimi Mziwanda nna haja gani ya
kucheat wakati mtoto ana kila kitu, kiukweli napenda mke wangu alivyojaa
jaa mie hoooooi,” aliandika kwenye picha nyingi ya Shilole. Naye Shilole kwenye picha
aliyoiweka kwenye mtandao huo akiwa na Nuh Mziwanda aliandika, “Ilove my
baby,” kudhihirisha upendo wake. Hakuna shaka kuwa uhusiano huo
umemwezesha Nuh Mziwanda kukuza jina lake na ameutumia vizuri
kujitambulisha zaidi.