Taarifa kutoka hospitali ya Mwananyamala ni kwamba leo wameshapokea wagonjwa 8 ambao wanahisiwa kuwa na vimelea vya ugonjwa huo wa Kipindupindu.
‘Hali
ya leo jana walikuwa 20 kwa hiyo leo wakaongezeka tena 8 kwa hiyo jumla
tuna wagonjwa 28 kati ya wagonjwa hao wagonjwa 9 wamepata nafuu
tumewaruhusu kwenda majumbani kwao na wagonjwa wengine 5 tumewapeleka
katika kambi ya kipindupindu Mburahati na wengine 5 majibu yao
yanaonesha (positive) kuwa wanavimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kwa
hiyo nao tunatakiwa leo hii kuwapelekea nao Mburahati’ – Dk Ngonyani
‘Na waliobaki 8 bado tunao katika
hospitali yetu ya Mwananyamala wanaendelea na uchunguzi na matibabu
hakuna mgonjwa yoyote aliyefariki siku ya leo‘ – Dkt. Ngonyani.
0 Comments