Kwa mara ya kwanza msanii wa muziki na filamu Bongo,Snura Mushi
amemwanika baba wa mtoto wake na kusema ndiye mumewe mtarajiwa wa kufa
na kuzikana.
Pichani ni msanii wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi pamoja na baba "Hunter" wa mtoto wake wa kike.
Akipiga stori na Ijumaa, Snura alisema baada ya kukaa kimya kwa muda
mrefu kutokana na ugomvi mkubwa waliokuwa nao yeye na mwanaume wake huyo
liyemtaja kwa jinamoja la Hunter, hivi sasa wamemaliza tofauti zao.
Mume mtarajiwa wa Snura akingusha pozi.
Alisema japo kuwa zamani aliapa kutorudiana naye baada ya kumuacha
akiwa mjamzito, sasa mambo ni shwari kwani amesharekebisha tofauti zao
na ndoa inanukia.
“Hunter ni mume wangu, nampenda na yeye nanipenda, kwasasa yupo
Mbeya kikazi ila siku akiwa mapumzikoni huja Dar na mimi wakati wingine
namfuata hukohuko, siku si nyingi tutafunga ndoa,” alisema Snura.
1 Comments
hongereni
ReplyDelete