
Askari wa jeshi la polisi wameshutumiwa kwa kuwajeruhi kwa risasi
wanawake wawili na kumshambulia kwa kipigo kiongozi wa chama cha
wananchi CUF wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Kutokana na shutuma hiyo dhidi ya askari wa jeshi
la polisi mkoa wa Kinondoni, mwandishi wa ITV amefika katika hospitali ya
Mwananyamala walikodaiwa kufikishwa watu hao watatu na kukutana kwanza
na mkurugenzi wa ulinzi wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Kinondoni
bwana Mwinyipembe Bakari akiwa amelazwa huku Bi Zawia Hamisi na Grace
Loy walilalamikia kupigwa risasi wakidaiwa kuondolewa haraka katika
hospitali ya Mwanayamala kutokana na usumbufu wa ujio wa vyombo vya
habari,ambapo licha ya mwandishi kuangaika kwa zaidi ya saa nne kuwatafuta
na kuwakuta eneo la Kisiwani wakihudumiwa na ndugu zao ambapo katika
mahojiano wamesema walikuwa wakisherekea shughuli ya ndugu yao na
walijua kuwa sheria hazuii kufanyika sherehe mchana.
Diwani wa kata ya Makumbusho bwana Harubu Mohamed
amesema wanawake hao walipigwa risasi huku ndugu zao nao wakija juu
wakihoji kwanini askari walitumia nguvu kubwa kiasi hicho na kushindwa
hata kupiga mabomu katika kutawanya watu hao?
Daktari aliyehudumia
wanawake hao dakta Thomson Minja amesema watu hao walipigwa na kitu
chenye ncha kali na kusababisha matundu yenye kina kirefu katika baadhi
ya sehemu ya miili yao
Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Camilius Wambura ambaye alikuwa kikazi nje ya ofisi amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kikundi hicho cha kanga moko moko walikuwa
wakifanya mambo ya aibu mbele za watu jambo ambalo sheria inazuia na
kwamba bado uchunguzi unaendelea ili kuweka wazi kama walipigwa na kitu
gani na askari yupi alihusika.
0 Comments