Baby Madaha mwigizaji wa filamu Swahiliwood
BABY Madaha mwigizaji wa kike wa filamu Bongo amejinadi kuwa yeye
ndio atakuwa Rais wa kwanza wa kike Tanzania, na ili kufanikisha ndoto
yake hiyo yupo katika Chuo kikuu huria akisoma masomo ya siasa na
amalizapo tu ataingia moja kwa moja katika kinyang’anyiro cha Urais.
“Nimeamua kusoma zaidi hasa siasa kwa ajili ya kugombea nafasi kubwa
ya Urais na si Ubunge, najiamini ninachofanya na nahitaji mambo makubwa
zaidi ya hapa nilipo, nitakuwa Rais wa kwanza mwanamke kuiongoza
Tanzania, nikiwa msanii,”anatamba Baby Madaha.
Msanii huyo hakusita kijibainisha kuwa ni mwanachama wa chama gani aliweka wazi kuwa yeye ni mwanaccm, Baby Madaha anasema nafanya hivyo kwa ajili ya kuwakomboa akina, watoto na wasanii ambao pamoja kazi zao kusifiwa lakini bado wamekuwa wakifa maskini.
0 Comments