Mwanadafada mkali wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Staa
wa kike anayefanya vizuri katika tasnia ya fillamu Yobnesh
Yusuph ‘Batuli’ amefunguka na kudai kuwa hajawahi kula hela ya
mume wa mtu na kama watu wanamhisi hivyo basi watakuwa
wanakosea sana…..
Batuli
alitoa kauli hiyo ili kuwathibitishia mashabiki wake juu ya
kauli mbovu za watu kuwa urembo wake unategemea mtaji wa
mwili wake ambapo amewajibu kwa kusema kuwa urembo na uzuri
wake unatokana na matunda ya kazi yake ya sanaa na kimsingi
anautumia huko kwa kuwa haoni faida ya kula hela ya mwanaume
kwani hajaifanyia kazi…..
“Amini
kuwa naendesha maisha yangu kwa misingi ya kazi zangu,
inawezekana wapo wanawake wanaoishi mjini kwa kutegemea mtaji wa
miili yao na si sanaa.
”
Kwa upande wangu hata Mungu ananiona kuwa kile ninachokipata
kupitia sanaa ndicho ninachokitumia kwenye matumizi yangu,” alisema Batuli
0 Comments