Advertisement

Responsive Advertisement

Binti aliyehukumiwa kifo nchini Sudan kwa kuolewa na Mkristo aachiliwa huru

Meriam Yehya Ibrahim Ishag aliadhibiwa kwa makosa mawili, zinaa na kuasi dini
  • Mwanamke aliyehukumiwa kifo nchini Sudan kwa kuasi dini ameachiliwa huru.
Wakili wake ameambia BBC kuwa mwanamke huyo aliyekiuka dini kwa kwa kuolewa na mwanamume mkristo aliachiliwa huru Jumatatu.


Hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Meriam Ibrahim,ilibatilishwa na mahakama ya rufaa, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna.
 
              
Meriam ameolewa na mwanamume mkristo na alihukumiwa kifo na mahakama ya kiisilamu kwa kosa la kuasi dini, baada ya kukataa kukana kuwa yeye ni mkristo.
 
Hukumu dhidi yake ilichochea viongozi wa kimataifa walioilaani wakisema inakiuka haki za binadamu.

Post a Comment

0 Comments