Stori:Na Mwandishi wetu
NGUZA Mbangu, mtoto mkubwa wa mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya, amesema mzazi wake pamoja na mdogo wake, Papii, ni lazima wataachiwa huru hivi karibuni.
NGUZA Mbangu, mtoto mkubwa wa mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya, amesema mzazi wake pamoja na mdogo wake, Papii, ni lazima wataachiwa huru hivi karibuni.
Mbangu, ambaye pia hufahamika kisanii kama Mashine, ambaye hivi sasa
ni mwinjilisti, alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipozungumza na gazeti
hili, akisema kuwa kutolewa jela kwa ndugu zake hao, kutawafanya
Watanzania kumsujudia Mungu kupitia tukio hilo.
“Amini nakuambia, Mungu amenipa maono, Babu Seya na Papii wako huru,
watatoka tu, kinachosubiriwa ni muda tu ambao hauko mbali, ni lazima
watatoka kwa sababu hawana hatia,” alisema Mbangu, ambaye pia
alihukumiwa kifungo cha maisha jela kama mzazi wake, lakini akaachiwa
wakati walipokata rufaa kwa mara ya kwanza mahakamani.
Alisema tukio hilo litakapotokea, litawafanya Watanzania wote
kumsujudia mwenyezi Mungu, kwa sababu litakuwa ni ishara ya uwezo wake
katika kutenda maajabu.
Babu Seya na Papii walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004
baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi
Mashujaa iliyopo Sinza. Hata hivyo, jitihada zao za kujinasua kwa mara
ya mwisho ziligonga mwamba hivi karibuni baada ya jopo la majaji watatu
kutupilia mbali maombi ya kuachiliwa huru baada ya kufanya mapitio ya
kesi hiyo iliyovuta hisia za watu wengi nchini.
source:eddy.com
0 Comments