HIVI NDIVYO MABASI YALIVYOGONGANA ENEO LA SABASABA NA KUDAIWA
KUSABABISHA VIFO VYA ZAIDI YA WATU WA 29 HADI SASA KWA MUJIBU WA TAARIFA
ZA AWALI.
Inaelezwa
kuwa ajali hiyo imehusisha magari matatu na kupoteza maisha ya watu
zaidi ya 30 na majeruhi zaidi ya 70 katika eneo la Sabasaba wilayani
Butiama.
Ajali hii imetokea majira ya saa 5 na nusu,Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara.
Amesema
ajali hiyo imehusisha basi la AM Coach lenye namba za usajili T736
AWJ likitoka Musoma kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi T677
CYC J4 Express likitoka Mwanza kwenda Tarime na gari jingine dogo aina
ya Nissan Corola P332 KKT likitoka eneo la Sabasaba yote yalikutana
kwenye mteremko yakitokea juu kwenda Darajani.
Katika hali ya kupishana kutokana na spidi yao hawakuweza
kupishana yakagongana na wakati huo gari hilo dogo lilipaki pembeni
baada ya kuona hali tete nalo likagongwa kwa nyuma likasukumwa na
kutumbukia mtoni.
Katika gari dogo kulikuwa na watu 8,wawili wamefariki dunia na majeruhi 36 kutoka kwenye mabasi hayo mawili nao wamefariki na majeruhi 80 wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mara.
Katika gari dogo kulikuwa na watu 8,wawili wamefariki dunia na majeruhi 36 kutoka kwenye mabasi hayo mawili nao wamefariki na majeruhi 80 wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mara.
MATUKIO KATIKA PICHA:
Habari za hivi punde zilizokifikia
chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba kuna ajali mbaya imetokea
katika eneo la sabasaba Darajani wilayani Butiama mkoani Mara.
WATU WAKIWA KATIKA ENEO LA TUKIO KUSHUHUDIA AJALI HIYO INAYOTAJWA KUWA MBAYA ZAIDI KUTOKEA ENEO HILO.
WAKAZI WA ENEO HILO NA MAENEO JIRANI WAKIWA KATIKA ENEO LA TUKIO.
MUNGU TUEPUSHE NA HAYA MAJANGA.
MIILI YA WANAUME WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO.
MIILI YA WANAWAKE WALIOFARIKI KATIKA JALI HIYO.
HII KWA MBALI NI FOLENI ILIKUWA ENEO HILO BAADA YA AJALI KUTOKEA.
JAMANI INASIKITISHA SANAAA
MIILI ILIYOBANWA NA VYUMA IKIWA BADO HAIJAONDOLEWA.