MWANAUME anayedaiwa kuwa ni kinara wa ubakaji jijini hapa, Said (30)
mkazi wa Mbauda, amenusurika kifo kwa kipigo kutoka kwa raia wenye
hasira baada ya kunaswa akitoka kumbaka denti wa kidato cha pili hadi
kupoteza fahamu.
Said anayetajwa kuwa ‘mwenyekiti’ wa kundi linalojihusisha na
ubakaji, alishambuliwa na wananchi hao baada ya yeye na wenzake watano
kukutwa kwenye nyumba inayodaiwa kuwa ya uhalifu iliyopo Muriet, Bon
City jijini hapa wakimfanyia kitendo hicho cha kinyama mwanafunzi huyo
mwenye umri wa miaka 14.
Mashuhuda wa tukio hilo, akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa, Francis Mbise
walieleza kuwa mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake hao walimbaka usiku kucha
msichana huyo aliyetajwa kwa jina moja la Jack, mkazi wa Kwamorombo
baada ya kufanikiwa kumrubuni kwa maneno na kumwingiza kwenye nyumba
hiyo.
Baada ya kufanya unyama huo usiku kucha, alfajiri mtuhumiwa huyo
alionekana akitoka ndani ya nyumba hiyo akiwa kifua wazi na kukimbia,
ndipo wananchi walipomtilia shaka na kumkimbiza na baada ya kukamatwa,
aliulizwa kama ni mwizi akakataa bali alitoka kufanya mapenzi na
msichana.
Mbise alisema kuwa wananchi hao waliongozana naye hadi kwenye nyumba
hiyo na kumkuta msichana huyo akiwa amelala hajitambui huku sehemu zake
za siri zikitoka damu.
Mwenyekiti huyo alisema walipomuhoji kwa nini alikuwa akikimbia,
alisema yeye alihofu kuwa msichana waliyembaka amepoteza maisha baada ya
kushtuka usingizini na kumwona hajitambui huku wenzake wakiwa hawapo.
Alisema mtuhumiwa huyo alikiri kuunda kundi la ubakaji lenye watu
watano likiongozwa na yeye huku wakigeuza makazi ya mmoja wa wahalifu
hao kuwa danguro la ubakaji. Ndipo wananchi hao walipoamua kumshushia
kipigo cha nguvu kabla ya polisi kufika na kumuokoa.
Watuhumiwa wengine walifanikiwa kukimbia na kutotambulika, lakini wananchi wa eneo hilo wanaendelea
kuwasaka.
Mtuhumiwa huyo alichukuliwa na polisi wenye silaha ndani ya gari aina ya
Land Rover lenye namba ya usajili PT 1177 huku akiwa ametapakaa damu
usoni.
CREDIT: GPL
0 Comments