ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimollo amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Kimollo, alisema
amechoshwa na ubabaishaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na
kushindwa kusimamia haki za wakulima wa kahawa.
Alisema anaamini kujiunga kwake na CHADEMA itakuwa fursa nzuri kwake
katika kupigania haki za wanyonge ambazo CCM kwa kipindi cha miaka 52
imeshindwa kufanya hivyo.
Alisema ameamua kujiunga na chama hicho, akiamini kuwa ndicho
kinaweza kusimamia demokrasia ya kweli, kitamsaidia katika vita yake ya
kumkomboa mkulima wa kahawa ambaye anadhulimiwa haki yake katika uuzaji
wa zao hilo.
“Nimejiondoa CCM kutokana na mtizamo wangu wa kupinga biashara ya
uuzaji wa kahawa usiofuata utaratibu, na ambao naamini usingeweza
kumsaidia mwananchi hususani kumkomboa katika dimbwi la umasikini
wilayani Mbozi,” alisema Kimollo.
Alisema aliwahi kutumikia nafasi ya ukuu wa wilaya katika wilaya za
Namtumbo, Makete na Mbozi kuanzia mwaka 1999 hadi 2012, ambapo alikoma
kufanya kazi hiyo kutokana na kutoelewana na baadhi ya viongozi wa CCM.
Kwa mujibu wa Kimollo, anaamini kuwa bado ana nguvu na uwezo, hivyo yuko tayari kuwatumikia wananchi ambao wanahitaji ukombozi.
Akimkabidhi Kimollo kadi ya CHADEMA, Mwanasheria wa chama hicho,
Tundu Lissu, alimpongeza akisema kitendo alichokifanya ni cha kijasiri
0 Comments