Advertisement

Responsive Advertisement

UCL: DROO RAUNDI YA MTOANO TIMU 16 JUMATATU DESEMBA 16

UEFA_CHAMPS_DRAWDROO ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, ili kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 itafanyika huko Nyon, Uswisi Jumatatu Desemba 16 kuanzia Saa 8 Mchana.
Katika Droo hiyo, Mabingwa Watetezi, Bayern Munich na Washindi wa Pili, Borussia Dortmund, wamo pamoja na wenzao wengine wawili wa Germany, Bayer Leverkusen na FC Schalke.
Ligi Kuu England inazo Timu 4 ambazo ni Mabingwa wake Manchester United, Man City, Chelsea na Arsenal.
Real Madrid, ambao wanasaka Taji lao la 10 Ulaya, wamo pamoja wenzao wa Spain, Barcelona na Atletico Madrid.
Italy imebakiwa na Timu moja tu ambayo ni AC Milan.
Miongoni mwa Timu hizo 16 ambazo zimo kwenye Droo, 4 zimetokea kwenye Raundi za Awali za Mchujo za UCL Msimu huu.
Kwa mujibu wa Kanuni za Droo, Timu zitawekwa kwenye Vyungu viwili, Chungu Namba 1 ni wale Washindi wa Makundi na Chungu Namba 2 ni Washindi wa Pili wa Makundi.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
CHUNGU NA 1-WASHINDI WA MAKUNDI:
-Manchester United FC (England)
-Real Madrid CF (Spain)
-Paris Saint-Germain (France)
-FC Bayern München (Germany, Mabingwa Watetezi)
-Chelsea FC (England)
-Borussia Dortmund (Germany)
-Club Atlético de Madrid (Spain)
FC Barcelona (Spain)
CHUNGU NA 1-WASHINDI WA PILI WA MAKUNDI:
-Bayer 04 Leverkusen (Germany)
-Galatasaray AÅž (Turkey)
-Olympiacos FC (Greece)
-Manchester City FC (England)
-FC Schalke 04 (Germany)
-Arsenal FC (England)
-FC Zenit (Russia)
-AC Milan (Italy)
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Droo hii itaendeshwa na Katibu Mkuu wa UEFA, Gianni Infantino, na Mkurugenzi wa Mashindano wa UEFA, Giorgio Marchetti, wakisaidiwa na Balozi wa Fainali za UCL 2013/14, Gwiji Luis Figo.
Kitakacho zingatiwa ni kuwa Timu toka Chungu Namba 1 itapambanishwa na Timu toka Chungu Namba 2 isipokuwa Timu zilizotoka Kundi moja au Nchi moja hazitaruhusiwa kukutana.
Pia, Washindi wa Makundi wataanza Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Ugenini hapo Februari 18/19 na 25/26 na kumalizia Nyumbani hapo Machi 11/12 na 18/19.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
UCHAMBUZI KWA TIMU 16:
WASHINDI WA MAKUNDI:
KUNDI A: Manchester United
WANAWEZA KUKUTANA NA: Galatasaray, Olympiacos, Schalke, Zenit, Milan
WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa wa England
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Wayne Rooney, Antonio Valencia Bao 2
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Raundi ya Mtoano Timu 16
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa x 3 (1968, 1999, 2008)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
B: Real Madrid
WANAWEZA KUKUTANA NA: Leverkusen, Olympiacos, Manchester City, Schalke, Arsenal, Zenit, Milan
WAMEINGIA UCL KAMA: Washindi wa Pili Spain
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Cristiano Ronaldo Bao 9
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Nusu Fainali
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa x 9 (1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
C: Paris Saint-Germain
WANAWEZA KUKUTANA NA: Leverkusen, Galatasaray, Manchester City, Schalke, Arsenal, Zenit, Milan
WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa, France
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Zlatan Ibrahimović Bao 8
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Robo Fainali
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Nusu Fainali (1995)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
D:  FC Bayern München
WANAWEZA KUKUTANA NA: Galatasaray, Olympiacos, Arsenal, Zenit, Milan
WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa Watetezi
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Mario Götze, Thomas Müller, Franck Ribéry, Arjen Robben Bao 3
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Mabingwa (2-1 v Borussia Dortmund, Wembley)
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa x 5 (1974, 1975, 1976, 2001, 2013)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
E: Chelsea FC
WANAWEZA KUKUTANA NA: Leverkusen, Galatasaray, Olympiacos, Zenit, Milan
WAMEINGIA UCL KAMA: Mshindi wa Tatu, England
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Demba Ba, Samuel Eto'o, Ramires, Fernando Torres Bao 2
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Makundi, baadae Europa League Mabingwa
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa (2012)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
F: Borussia Dortmund
WANAWEZA KUKUTANA NA: Galatasaray, Olympiacos, Manchester City, Zenit, Milan
WAMEINGIA UCL KAMA: Washindi wa Pili, Germany
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Robert Lewandowski Bao 4
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Fainali (1-2 v FC Bayern München, Wembley)
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa (1997)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
G: Club Atlético de Madrid (ESP)
WANAWEZA KUKUTANA NA: Leverkusen, Galatasaray, Olympiacos, Manchester City, Schalke, Arsenal, Milan
WAMEINGIA UCL KAMA: Washindi wa Tatu, Spain
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Diego Costa 4
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: UEFA Europa Ligi Raundi ya Timu 32
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Washindi wa Pili (1974)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
H: FC Barcelona
WANAWEZA KUKUTANA NA: Leverkusen, Galatasaray, Olympiacos, Manchester City, Schalke, Arsenal, Zenit
WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa, Spain
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Lionel Messi Bao 6
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: semi-finals
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa x 4 (1992, 2006, 2009, 2011)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
WASHINDI WA PILI WA MAKUNDI:
A: Bayer 04 Leverkusen
WANAWEZA KUKUTANA NA: Real Madrid, Paris, Chelsea, Atlético, Barcelona
WAMEINGIA UCL KAMA: Washindi wa Tatu, Germany
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Simon Rolfes Bao 3
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: UEFA Europa Ligi Raundi ya Timu 32
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Washindi wa Pili (2002)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
B: Galatasaray AÅž
WANAWEZA KUKUTANA NA: Manchester United, Paris, Bayern, Chelsea, Dortmund, Atlético, Barcelona
WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa, Turkey
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Umut Bulut Bao 3
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Robo Fainali
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Nusu Fainali (1989)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
C: Olympiacos FC (GRE)
WANAWEZA KUKUTANA NA: Manchester United, Real Madrid, Bayern, Chelsea, Dortmund, Atlético, Barcelona
WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa, Greece
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Kostas Mitroglou Bao 3
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Makundi baadae Europa Ligi Raundi ya Timu 32
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Robo Fainali (1999)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
D: Manchester City FC
WANAWEZA KUKUTANA NA: Real Madrid, Bayern, Paris, Atlético, Barcelona
WAMEINGIA UCL KAMA: Washindi wa Pili, England
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Sergio Agüero Bao 6
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Makundi
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Makundi
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
E: FC Schalke 04 (GER)
WANAWEZA KUKUTANA NA: Manchester United, Real Madrid, Paris, Atlético, Barcelona
WAMEINGIA UCL KAMA: Nafasi ya 4, Germany
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Julien Draxler Bao 3
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Raundi ya Timu 16
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Nusu Fainali
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
F: Arsenal FC
WANAWEZA KUKUTANA NA: Real Madrid, Paris, Bayern, Atlético, Barcelona
WAMEINGIA UCL KAMA: Nafasi ya 4, England
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Olivier Giroud, Aaron Ramsey, Jack Wilshere 2
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Raundi ya Timu 16
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Washindi wa Pili (2006)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
G: FC Zenit
WANAWEZA KUKUTANA NA: Manchester United, Real Madrid, Paris, Bayern, Chelsea, Dortmund, Barcelona
WAMEINGIA UCL KAMA: Mshindi wa Pili, Russia
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Hulk, Aleksandr Kerzhakov Bao 2
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Makundi baadae Europa Ligi Raundi ya Timu 16
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Raundi ya Timu 16
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
H: AC Milan
WANAWEZA KUKUTANA NA: Manchester United, Real Madrid, Paris, Bayern, Chelsea, Dortmund, Atlético
WAMEINGIA UCL KAMA: Nafasi ya Tatu, Italy
MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Mario Balotelli Bao 2
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Raundi ya Timu 16
MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwas x 7 (1963, 1969, 1989, 1990, 1994, 2003, 2007)

Post a Comment

0 Comments