Kinywaji cha coca cola kimeendelea kuwa maarufu duniani lakini utafiti
mpya umeonyesha kuwepo uhusiano wa kunywa sana kinywaji hicho na
matatizo ya uzazi kwa wanaume.
Kwa mjimu wa utafiti huo uliochapichwa
kwenye Jarida la Epidemiology la Marekani, wanaume wanaokunywa zaidi ya
lita moja ya coca cola kwa siku wanakabiliwa na hatari ya kuwa tasa.
Wanaume waliotumia kinywaji hicho walikuwa na upungufu wa aslimia 30 ya
mbegu za uzazi zilizohesabiwa, ikilinganishwa na wale ambao
hawakutumia. Wanaume hao walionekana kuwa na matatizo ya uzazi zaidi
kuliko wasiokunywa coca cola.
0 Comments