STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed
‘Shilole’ amefunguka kuwa katika uhusiano wa kimapenzi hajawahi kuachwa
bali huwa anaacha mwenyewe.
Akistorisha na mwanahabari wetu, Shilole alisema tangu aanze kuwa na
uhusiano, amekuwa bingwa wa kupiga ‘vibuti’ wanaume ambao hawaeleweki.
“Ukweli sijui nina nini ila naamini Mungu amenipa kitu cha pekee kwa
sababu naweza kumuacha mwanaume kwa kumtukana lakini akataka kurudi,
sijawahi kuachwa,” alisema Shilole.
0 Comments