"Ni
muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mienendo ya mume wangu
kutokana na tabia yake kubadilika sana siku za hivi karibuni,
nikabaini kuwa kuna msichana anawasiliana naye kwa kutumiana meseji za mapenzi, sikuwa na haraka nikaamua kufanya uchunguzi wangu kimyakimya"
"Wiki
iliyopita mume wangu akiwa amekwenda kuoga akasahau kuzima
simu yake,na siyo kawaida yake kuacha simu yake bila
kuizima,mara meseji ikaingia,nikaangalia nikaona jina la mtumaji
amesevu Lulu, moyo ukalipuka"
Ndivyo
alivyoanza kuongea mama mmoja wa makamo anayefanyakazi katika
ofisi moja nyeti katikati ya jiji la Dar alipokuja kuongea na
mwandishi wetu wiki iliyopita baada ya ndoa yake kuingiliwa
na mdudu mbaya....
Akiongea
kwa masikitiko makubwa, mama huyo ambaye hakupenda kutaja jina
lake kutokana na unyeti wa kazi anayoifanya, alidai kuwa
msichana huyo anayetaka kuiharibu ndoa yake yenye miaka 25
jina lake ni Elizabeth Michael....
Mama
huyo alidai kuwa jina hilo alilibaini baada ya kukuta meseji
za mapenzi kwenye simu ya mume wake na yeye kuamua
kuifuatilia namba hiyo kwa kufanya kama anataka kumtumia pesa
msichana huyo na kukugundua jina hilo....
Akiongea
kwa upole, mama huyo alidai kuwa katika simu ya mume wake,
jina la mtumaji lilikuwa Lulu, lakini alipofanya uchunguzi wake
wa kujifanya kama anatuma pesa kwa namba ya msichana huyo
ndipo alipobaini kuwa mmiliki wa namba hiyo ni Elizabeth
Michael...
Mwandishi
alimuuliza mama huyo kama anadhani kuwa msichana huyo
anayetaka kuiharibu ndoa yake ni muigizaji maarufu wa filamu
hapa nchini Elizabeth Michael "Lulu", lakini alikataa kuthibitisha
hilo kwa madai kuwa tangu siku hiyo namba ya binti huyo
imekuwa haipatikani....
"Baada
ya kugundua siku ile , nilichukua simu yake na kutaka
kuwasiliana naye ili niweze kumuonya mwenyewe kimyakimya kwa
wakati wangu, wala sikuwa na lengo la kuja kwenye vyombi vya
habari , lakini sikuwahi kumpata hewani tena kila nilipojaribu
kumpigia"Alisema na kuongeza:
"Huenda
mume wangu alishtikia kuwa nimeona ujumbe ule, kwa sababu mimi
nilipoisoma meseji ile sikuifuta, ili akiona meseji imesomwa
aelewe nimeshajua kila kitu, pengine ndiye aliyemwambia binti
huyo abadili namba yake"
Mwandishi
alimuomba mama huyo ampatie namba ya huyo msichana ili kuweza
kujua kama ni Lulu muigizaji ama siyo ( mwandishi anazijua
namba zote za Lulu ), lakini namba hiyo ni tofauti na
anazotumia Lulu Mwenyewe....
Mwandishi
alipojaribu kama kumtumia pesa msichana huyo, jina lililotokeza
ni Elizabeth Michael, na alipojaribu kuipiga namba hiyo ilikuwa
haipatikani hewani....
Juhudi
za kumsaka Lulu ili kuona kama anaitambua namba hiyo
hazikuzaa matunda kutokana na namba zake mbili kutopatikana na
nyingine ikiita bila kupokelewa....
Angalizo:
Baadhi
ya wasichana wa mjini wamekuwa wakitumia majina ya wasanii
maarufu katika nyendo zao ili kuwatapeli watu. Miongoni mwa
njia wanazotumia ni pamoja na kujisajili kwenye mitandao ya
kijamii kwa majina ya watu maarufu ili kuwatapeli watu.
0 Comments