WAKATI msanii wa kizazi kipya anayefanya vizuri kwa sasa na kujizolea tuzo 7 alizokuwa anawania kupitia Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014, Naseeb Abdul 'Diamond akiibuka shujaa Mlimani City jijini Dar ambako hafla hiyo ya utoaji tuzo ilifanyika, usiku huo ulikuwa mbaya kwa mpenzi wake wa zamani,Jokate Mwegelo ambaye huenda alijuta kufika mahali hapo....
Matukio ambayo yalimnyong'onyesha Jokate ni namna ambavyo msanii huyo na mpenzi wake Wema Sepetu walivyokuwa wakionyesha mahaba mazito ukumbini ilihali yeye akishuhudia....
Katika hali ya kushangaza, Diamond na Wema kila walipokuwa wakichukua tuzo walikuwa wakizunguka nyuma ya jukwaa ambako alikuwepo Jokate na kuzibwaga tuzo hizo mezani kisha kukandamiza 'Denda Live' mbele yake kiasi cha kumfanya mwanamitindo huyo ainame kwa Aibu....
Diamond alionekana kumpotezea vibaya mwandani wake huyo wa zamani huku Wema akijikosha kwa kumpa mkono wa kejeli hali iliyomfanya Jokate akose raha wakati wote alipokuwa akiwaona wapenzi hao....
Matukio ambayo yalionekana kumchoma zaidi moyoni ni jinsi Wema alivyokuwa akimvuta Diamond na kubadilishana mate mbele yake jambo ambalo lilitafsriwa kama ni kumfanyia makusudi mwanamitindo huyo ambaye kipindi cha nyuma alifanikiwa kuleta tafrani kubwa na kuligawa vipande vipande penzi la wawili hao kiasi cha Wema kulalamika redioni....
Hali ya Jokate kukumbwa na mfadhaiko ilizua minong'ono kwa baadhi ya mashuhuda kwamba Diamond na Wema waliamua kukata kabisa mzizi wa fitina kwa Jokate na kuudhihirishia umma kuwa ya kale ni dhahabu...
"Maskini Jokate, ona anavyofanyiwa na Wema,inauma sana moyoni.Unajua mwanaume kama umewahi kulala naye hata mara moja ukiona anafanya mahaba na mwanamke mwingine inauma" Alisikika staa mmoja akiteta na mwezake
Hadi hafla hiyo inamalizika,Jokate aliganda kwenye kiti akiwa amepooza tofauti na ilivyo kwa staa huyo anapokuwa katika matukio makubwa kuwa na makeke
0 Comments