Ukiachana na burudani kutoka kwa wanamuziki mbalimbali kwenye
hafla ya kukabidhi tuzo za muziki za Kilimanjaro, burudani zaidi ilikuwa ni maneno kutoka kwa MC
ambaye pia ni mwigizaji sanaa ya vichekesho Mpoki ambaye alikuwa anawakonga
nyoyo waliohudhuria kwa kauli zake tata ambazo zilikuwa zinawavunja mbavu. Na hizi
ni baadhi ya kauli na misemo ambayo iliwavunja watu mbavu.
- Tusiaandikie penseli wakati penny aliyekuwa wa Diamond yupo.
- Kama usiku wa jana ulilala na haukuota basi leo lala na mbolea utaota.
- Big up kwa wasichana wote ambao wamevaa vimini kwa sababu walijua kuwa mlimani city hakuna mbu, ahsante sana kwa kwenda na wakati.
- Wema mamaa magazeti
- Kuchuna buzi na kuchanganya mabwana ni kipaji pia
- Ukiona panya anakatisha katisha sebuleni ujue anataka kujulikana.
- Kirefu cha HIV ni Hatari Imeingia Vitandani.
- Hivi ukiwa mcheza shoo lazima ujichubue?
- Na mimi pia ni dokta lakini wa magonjwa ya kike
0 Comments