Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya |
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mihangwa Maguta (30) mkazi wa kijiji cha Nyenze Matelu kata ya Mwadu- Luhumbo tarafa ya Mondo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ameuawa baada ya kupigwa kwa jiwe kubwa kichwani na watu anaodaiwa kuwadhulumu pesa za mauzo ya madini ya almasi.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya tukio hilo limetokea jana (Mei 7,2014) saa moja asubuhi katika kijiji hicho cha Nyenze Matelu wilayani Kishapu.
Imedaiwa chanzo cha mauaji hayo inasadikiwa kuwa marehemu amewadhulumu wenzake watatu pesa za mauzo ya madini ya almasi.
Tayari jeshi la polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watuhumiwa wa mauaji hayo akiwemo Makoye Manyenze aliyesababisha kifo cha Mihangwa Maguta.
Watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa na polisi ni Abdalah Idd (32) na Ally Omary (22) wote wakiwa ni wakazi wa kijiji cha Nyenze Matelu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
0 Comments