Advertisement

Responsive Advertisement

LULU AIOMBA BASATA IRUHUSU KUFANYA MOVIE NUSU UTUPU ILI KUENDANE NA SOKO LA KIMATAIFA!!!


DIVA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameziomba mamlaka zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii waigize nusu utupu ili kuendana na soko la kimataifa.

Akitetea hoja yake mbele ya paparazi wetu, staa huyo aliyeitendea haki filamu ya Foolish Age alitolea mfano Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa Lupita Nyong’o ambayo alicheza akiwa nusu utupu.

“Wanasema hatufuati maadili wakati kuna muvi ambazo zipo theatre na watu wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tuna takiwa tuweke vitu wazi, wasibane sana,” alisema Lulu.

Post a Comment

0 Comments