Kama ilivyo siku zote yanapofanyika mashindano lazima kuwe na pande mbili, moja ikiwa ni ya wale watakaofurahia matokeo kutokana na kushinda na upande wa wale ambao hawatafurahia kutokana na kushindwa na mara nyingine kutoridhishwa kabisa na matokeo.
Producer aliyetengeneza hit ya ‘Number One’ ya Diamond Platnumz,
Sheddy Clever ni miongoni mwa wale ambao hawakubahatika kunyakua tuzo za
KTMA 2014 Jumamosi iliyopita.
Hiki ndicho kilio chake baada ya kutopata Tuzo:
“Ndugu zangu watanzania naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru
saana kwa wote walionipigia kura na ata ambae hakunipigia kura ila kwa
namna moja amechangia mimi kufika hapa nilipo pia naomba niwashukuru
radio na tv zoote ndani na nje ya nchi ya TANZANIA.
"Sasa ndugu zangu
hivi nitashindwa vp kuchukua tuzo ya producer bora wa mwaka wakati
nimetayarisha wimbo uliochukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka na ni wimbo
ambao umemfanya Msanii @diamondplatnumz aweze kuchukua tuzo zaidi ya 5
#ktma
"Hii inaonesha kua muziki we2 watanzania bado unahitaji elimu ya
kutosha ila cna maana mbaya hapana bt nawashukuru saaana #ktma kwa kazi
walio fanya pia nawashukuru wasanii wote niliofanya nao kazi na ata wale
wenye ndoto za kufanya kazi na mimi.
"Hongera saana @diamondplatnumz
kwani muziki wetu unakua pia tusubiri tuzo za MTVBASE na Imani zitakuja
nyumbani. Cna mengi ndugu zangu watanzania nawapenda saana”.
Sheddy Clever alikuwa akiwania kipengele cha mtayarishaji bora wa
mwaka-kizazi kipya, tuzo iliyonyakuliwa na Man Water wa Combination
Sound
Categories:
0 Comments