Shakira amekuwa mtu wa kwanza duniani kwenye mtandao wa Facebook kupata Likes milioni 100 katika ukurasa wake.
Nyota huyo wa muziki kutoka nchini Columbia amevunja rekodi hiyo siku
nne tu baada ya kufanya onyesho katika fainali za michuano ya kombe la
dunia nchini Brazil.
Shakira aliyemzidi Rihanna kama Star wa kwanza Facebook mwezi Machi
mwaka huu akiwa na watu milioni 86.8 amesema kuwa anajisikia fahari
kubwa kufikia rekodi hiyo kwasababu hiyo ni sehemu pekee
inayomuunganisha na mashabiki wake kutoka sehemu mbalimbali duniani.

0 Comments