Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John P. Magufuli, (Mb) amesema kuwa
Serikali itajenga barabara kwa kiwango cha lami kuunganisha Wilaya ya
Mbinga hadi Mbamba bay Wilaya mpya ya Nyasa itakayokuwa na urefu wa
Kilometa 67.
Dkt. Magufuli aliyasema hayo jana alipokuwa anahutubia mamia ya Wakazi wa Nyasa kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa miguu Mbamba bay, mara baada ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kiwete kufungua Madaraja pacha ya Ruhekei A, B na C yaliyogharimu kiasi cha Tsh. bil.4.
“Mhe. Rais napenda kutamka hapa kuwa kama tumeweza kujenga mtandao wa barabara za lami zaidi ya km. 11,000 nchi nzima hatuwezi kushindwa kujenga km. 67 kwa kiwango cha lami.
Waziri Magufuli aliongeza kuwa tayari Wizara ya Ujenzi imetenga fedha kiasi cha Shilingi Bil. 2.3 katika mwaka wa fedha 2014/15 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo katika kiwango cha lami.

0 Comments