Arsenal wameambiwa
Juan Quintero, 21, ataruhusiwa tu kuondoka Porto iwapo kifungu cha pauni
milioni 32 cha uhamisho kitatenguliwa (Daily Express) Manchester United
wanakaribia kufanikisha uhamisho wa pauni milioni 20 wa
Mats Hummels, 25, huku Borussia Dortmund wakiwa na matumaini ya kuziba
pengo hilo kwa kumchukua Tiago IIori, 21, kutoka Liverpool kwa mkopo
(Daily Mirror), rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amethibitisha kuwa
klabu yake inamtaka kiungo wa Manchester United Marouanne Fellaini, 26,
ingawa kuna wachezaji wengine pia inawafuatilia (Daily Telegraph),
Liverpool inatazama kuwachukua mabeki kutoka Spain Alberto Moreno, 22,
wa Sevilla na Javier Manquillo, 20 kutoka Atletico Madrid (Daily Star),
West Ham wamekuwa na mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea
Samuel Eto'o, 33, na pia Hugo Almeida, 30 kutoka Besitkas (Times), kocha
wa Atletico Madrid Diego Simione yuko tayari kupanda dau kumchukua
kiungo wa Manchester United Shinji Kagawa, 25 (Daily Express), QPR
wameelekeza macho yao kumfuatilia kiungo Morgan Amalfitano, 29 kutoka
Marseille, aliyeichezea West Brom kwa mkopo msimu uliopita (Daily Mail),
Arsenal wanamfuatilia beki wa Real Madrid Alvaro Arbeloa iwapo Thomas
Vermaelen ataondoka Emirates (AS), Arturo Vidal wa Juventus amepita
katika vipimo vya afya na anasubiri makubaliano ya mwisho kusaini
mkataba na Manchester United (Metro), kiungo wa Porto Juan Quintero
amesafiri kwenda London kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Arsenal
(Marca).
0 Comments