MENEJA mpya wa klabu ya
Manchester United ameanza vibaya kampeni zake za Ligi Kuu baada ya
kushuhudia kikosi chake kikitandikwa mabao 2-1 dhidi ya Swansea city
katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Old Trafford mchana wa
leo. Wageni Swansea ndio waliokuwa wa kwanza kuchukuliwa wavu wa United
kwa bao lililofungwa na Ki Sung-yueng katika dakika ya 28 lakini bao
hilo lilisawazishwa muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili kupitia
kwa nahodha wake Wayne Rooney. Swansea walifunga bao lao la ushindi
katika dakika ya 72 kupitia kwa Gyfi Sigurdsson hivyo kuifanya timu hiyo
kupoteza mchezo wake wa ufunguzi nyumbani kwa mara ya kwanza toka mwaka
1972. United walionekana kushindwa kabisa kutengeneza mipango ya
kusawazisha bao hilo hatua ambayo mashabiki wake walionnekana kukata
tamaa na kuanza kuondoka mapema uwanjani kabla ya mchezo
kumalizika. Mashabiki wa United duniani kote kabla ya mchezo walionekana
kuwa na imani kubwa na kikosi chao toka alipotua Van Gaal akichukua
mikoba ya David Moyes ambaye alifanikiwa kushinda mechi zake zote za
kirafiki alizocheza.
0 Comments