MISS
Tanga 2011, Zubeida Seif ametaka kuzichapa kavukavu na mwenzake
aliyefahamika kwa jina moja la Kelly kisa kikiwa ni mkali wa wimbo wa
Mwana, Ali Saleh Kiba.
Tukio hilo lililoacha watu midomo wazi lilitokea juzikati katika baa
moja iliyopo maeneo ya Mwenge, Dar ambapo ubishi ulianza baada ya
Zubeydah kutetea kuwa Ali Kiba anajua kuimba kuliko Nasibu Abdul
‘Diamond’ huku mwenzake akimpinga ndipo mtiti ulipoibuka.
Mkali wa wimbo wa Mwana, Ali Saleh Kiba.
“Wewe umezidi, unataka kusikilizwa wewe
wakati ukweli unajulikana, acha hizo, ngoja nikuoneshe,” alisikika miss
huyo ambaye sasa anatamba na wimbo wa Zaidi ya Wale.
Bahati nzuri watu waliokuwepo eneo hilo waliwaamulia, wakatulia.
0 Comments