Nabii Yaspi akijibu maswali ya wanahabari wa GPL (hawapo pichani), mbele ya kamera za Global TV Online.
Nabii
Yaspi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa GPL kutoka kulia
ni Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist, Mkuu wa Kitengo
cha Teknolojia ya Habari (IT), Clarence Mulisa na Mhariri wa Gazeti la
Ijumaa, Amran Kaima.
Nabii Yaspi akiwa katika picha na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.
Nabii Yaspi akipozi na Mwandishi Nyemi Chilongani wa GPL.
NABII wa Kanisa la Ufunuo kwa Watu Wote lililopo eneo la Yombo
Buza-Kipera jijini Dar, Yaspi Paul Bendera, ametembelea ofisi za Global
Publishers LTD zilizopo Mwenge, Bamaga, Dar hivi punde na kutoa utabiri
kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Ebola hapa nchini.
Katika utabiri wake, Nabii Yaspi amesema watu 50 watapoteza maisha kwa ugonjwa huo, wakiwemo madaktari wawili na mbunge mmoja.
Nabii huyo amesema kuwa kwa sasa ugonjwa huo bado haujaingia nchini
lakini unaweza kuingia muda wowote kuanzia sasa iwapo watu wataendelea
kutomtii Mwenyeji Mungu.
0 Comments