Naibu
Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika,Godfrey Zambi amenusurika kupata
kipigo kutoka kwa wakulima wa zao la pamba katika kijiji cha Marekano
wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kwa madai ya kutoridhishwa na majibu
aliyoyatoa juu ya mbegu za pamba zisizo na manyoya(Quton)kutoota katika
msimu uliopita wa kilimo.
Tukio
hilo limetokea juzi kijijini hapo wakati Naibu Waziri huyo alipofanya
ziara ya kushitukiza ya kutembelea vituo vinavyonunua zao hilo katika
wilaya hiyo ili kukagua mizani zinayotumika kupimia zao hilo kutoka kwa
wakulima.
Wakati
akitoa majibu kwa wakulima ambao walikusanyika ghafla wakati akikagua
Mizani hiyo katika moja ya kituo kilichopo kijijini hapo ambao walihoji
ni kwa nini serikali iliwalazimisha kununua mbegu hizo ambazo hazikuota
pamoja bei ya kununulia zao hilo, naibu waziri huyo alijikuta
akinusurika kupigwa na wananchi hao baada ya kuwapa majibu
ambayo hayakuwaridhisha
0 Comments