KLABU ya Barcelona
imepata ahueni kwa kurejea mazoezini kwa nyota wa kimataifa wa Brazil,
Neymar baada ya kupona majeruhi ya mgongo yaliyokuwa
yakimsumbua. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikwamia katika
hatua ya robo fainali katika michuano ya Kombe la Dunia kufuatia
kugongana na beki wa kimataifa wa Colombia Camilo Zuniga katika mchezo
uliozikutanisha timu hizo. Lakini baada ya kupita wiki sita, Neymar sasa
amejiunga na kikosi kizima cha Barcelona kwa ajili ya mazoezi leo akiwa
sambamba na nyota mpya Jeremy Mathieu na Xavi ambao nao walikuwa
majeruhi. Hata hivyo beki mpya aliyesajiliwa Thomas Vermaelen ambaye
ametokea Arsenal kwa kitita cha paundi milioni 15 ameshindwa kufanya
mazoezi na wenzake leo na badala yake alifanyiwa vipimo zaidi kuangalia
majeruhi yanayomsumbua ambayo aliyapata katika Kombe la Dunia. Barcelona
inaanza kampeni zao za La Liga Agosti 24 dhidi ya Elche na huo utakuwa
mchezo wa kwanza kwa kocha Luis Enrique.
0 Comments