JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Mnamo mwezi wa Machi 2014 Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii ilipokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ugonjwa wa
Ebola katika nchi za Afrika Magharibi ambao ulianzia katika ya Guinea na
kusambaa katika nchi za Siera Leone, Liberia na Nigeria. Hadi tarehe 31 Julai, 2014 idadi ya wagonjwa ilikuwa 1323
na vifo 729.
Ugonjwa wa Ebola husababishwa na virusi vya Ebola. Dalili
zake ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa, na
vidonda kooni. Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele
vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa
damu ndani na nje mwilini. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati
ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi.
Ugonjwa wa Ebola unaambukiza kwa kasi na unaenea kati ya
mtu na mtu kwa:
o
kugusa
damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo
o
kugusa
maiti wakati ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huu.
o
kugusa
wanyama walioambukizwa Mizoga na wazima kama vile sokwe na swala wa msitu.
Aidha Ugonjwa wa Ebola hauna tiba wala chanjo.
Hadi
sasa hapa nchini Tanzania hakuna mgonjwa yoyote aliyehisiwa au kuthibitishwa
kuwa virusi vya Ebola.
Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii imeandaa mikakati ya kuzuia ugojnwa huu usiingie hapa nchini na
ikiwa utaiingia uweze kudhibitiwa kabla haujasambaa. Mikakati hiyo ni pamoja na:
o
Kuunda
kikosi kazi (Task Force) kinachohusisha
wajumbe mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na WHO,
UNICEF, USAID na CDC kwa ajili ya kuweka
mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huu ikwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji
wa mpango wa dharura wa kukabiliana na Ebola ambao tayari umeandaliwa.
o
Kutoa
taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Makatibu Tawala na Waganga
Wakuu wote wa Mikoa. Aidha taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza
kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Fact
sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli,
na na namna ya kuwahudumia wagonjwa.
o
Kuboresha
ufuatiliaji na utambuzi wa ugonjwa katika maeneo ya viwanja vya ndege na
mipakani ili kuweza kubaini wasafiri watakaoonyesha dalili za ugonjwa au wenye
viashiria hatari. .
o
Miongozo
ya utoaji elimu imeandaliwa ikiwemo Vipeperushi. Aidha watalaamu wa Afya wanaendelea
kutoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu kupitia vyombo mbalimbali
vya habari ili endapo ugonjwa huo ukitokea uweze kutolewa taarifa mapema
o
Vifaa
kinga (Personal Protective Gears) vipo
vya kutosha na Wizara imeanza kuvisambaza kutoka bohari za kanda za MSD na kuzipeleka
kwenye vituo vya kutoa huduma za afya ili watumishi wa afya waweze kutumia
iwapo mgonjwa atajitokeza. Aidha idadi itaongezwa kadiri ya mahitaji
yatakavyojitokeza.
o
Wizara
imebainisha vituo vya kutolea huduma kwa mikoa yote iwapo endapo ugonjwa huu
utatokea hapa nchini. Aidha katika vituo hivi, vifaa kinga pamoja na madawa
vimeshaandaliwa.
o
Kuwasiliana
na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa maendeleo ili kuweza kupata msaada wa
mahitaji mbalimbali kama yalivyoainishwa kwenye mpango wa dharura wa kukabliana
na Ebola ulioandaliwa.
Hitimisho
Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu ila kuendelea kuchukua
tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu. Ugonjwa
wa Ebola unaweza kuzuilika. Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu ni:-
o
Kuepuka
kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola
o
Wananchi
wanatahadharishwa kuepuka kushughulikia
maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za Ebola; badala yake watoe taarifa kwa
uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri.
o
Wananchi
waepuke mila na desturi zinazoweza
kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola.
o
Zingatia usafi wa mwili tabia na kiroho.
o
Kutoa
taarifa mapema kwa viongozi wa Serikali
na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za Ebola.
o
Kuwahi
katika vituo vya huduma za Afya pale mtu
anapoona dalili za ugonjwa huu.
Wizara itaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali kuimarisha ufuatiliaji ili
kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini.
Charles
A. Pallangyo
Katibu Mkuu
01
Augus,t 2014
0 Comments