Mke wa kigogo (Mugaka),Bi. Leah aliyefanyiwa unyama na mumewe.
KIGOGO wa shirika moja la kimataifa
linalojishughulisha na watoto yatima, tawi la mkoani Pwani, Tanzania
aliyetajwa kwa jina moja la Mugaka, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya
miaka 35 hadi 40, ametupwa rumande akituhumiwa kumchoma kisu na kumtoa
manundu mkewe, Leah (28).
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri wilayani
Kisarawe, Pwani mwishoni mwa wiki iliyopita. Kwa mujibu wa habari
zilizopatikana, chanzo cha unyama huo kinashangaza huku madai ya Mugaka
ambaye ni afisa mshauri wa shirika hilo yakisema mkewe huyo amekuwa
akimjazia choo kwa kuwa tangu amuoe miaka mitatu iliyopita, ameshindwa
kumzalia mtoto.
Habari ziliendelea kudai kwamba shirika analofanyia kazi Mugaka
linalosimamiwa na mfuko wa rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton.
Madai mazito yalishushwa kwamba Mugaka amekuwa akimnyanyasa mkewe kwa
sababu hiyo, kiasi cha kumtolea maneno ya kejeli, dharau, kashfa huku
akimshushia kipigo ‘hevi’.
Ilisemekana kwamba ilifika wakati hali ikawa mbaya kiasi cha baadhi
ya majirani kumshauri Mugaka kuachana naye kama anaona hamfai.
Ilisemekana kwamba chanzo cha kufanyiwa unyama huo na kujeruhiwa na kisu
ni madai ya mwanaume huyo kuwa alitumiwa ujumbe mfupi kwenye simu yake,
akiambiwa kuwa mkewe alikuwa akimsaliti kwa kutembea na watu wa nje,
wakiwemo polisi.
Ilidaiwa kwamba mkewe alikataa madai hayo na kumtaka mumewe kuitoa
namba ya simu iliyotuma ujumbe huo ili wampigie palepale wakiwa wote,
lakini jamaa huyo alikataa na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili
huku akimchoma na kisu pajani.
Jirani wa mtuhumiwa aliyeomba hifadhi ya jina alidai kwamba Mugaka
amekuwa akimpiga, kumtesa, kumdhalilisha mkewe mara kwa mara huku
akisikika kumweleza kuwa ipo siku atamuua.
Polisi cha Kisarawe, OCD Issa na kumtaarifu tukio hilo ambapo askari wake walifika na kuizingira nyumba ya mtuhumiwa huyo na ilipofika majira ya saa 11:00 alfajiri walifanikiwa kumtia mbaroni. Kigogo huyo amefunguliwa mashitaka ya shambulio la kudhuru mwili na
kujeruhi kwa kisu katika jalada lenye kumbukumbu namba KIS/RB/964/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU NA KUJERUHI MWILI akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
0 Comments