Hapa wananchi wakiwachoma moto mbwa hao
……………………………………………………….
Na Bazil Makungu Ludewa na Nickson Mahundi
Wananchi wa kata ya Ludewa
wameungana pamoja kufanya maandamano ya kushinikiza mbwa waliomuua mtoto
na kumtafuna wanauawa baada ya mmiliki wa mbwa hao kutishia kuwashtaki
watakao husika kuwaua mbwa wake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
katika mkutano wa dharula ulioitishwa na Diwani wa kata ya Ludewa Mama
Monica Mchilo walisema Mbwa hao wamekuwa tishio kwa muda mrefu kwani
wameshateketeza mifugo mingi wakiwemo mbuzi lakini cha kushangaza kila
wanapolipeleka suala hilo katika vyombo vya dola mmiliki huwaeleza
walete ushahidi.
Kutokana na hali hiyo tata mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha ameviagiza vyombo husika ikiwemo idara ya kilimo na mifugo, jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote anayehusika na tukio hili akiwemo mmiliki wa mbwa hao Bosco Thobias Lingalangala kwa sababu hakuna mtu aliye juu ya sheria.
Juhudi za kumpata mmiliki wa mbwa hao Lingalangala(BOLI) ambaye aliwahikuwa kiongozi wa klabu ya yanga miaka ya nyuma hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kutopokelewa na baadaye kuzimwa kabisa.
Hali hiyo imejitokeza tena kwa
mmiliki wa mbwa hao alipoelezwa kuwa wamefanya mauaji na kumla mtoto wa
darasa la tatu katika shule ya msingi Ludewa mjini aliyefahamika kwa
jina la Ibrahim Chipungahelo(9)aliwataka wananchi kuleta ushahidi licha
ya kuwa Askari wa jeshi la polisi kwa kutumia silaha na kuuokoa mwili wa
mtoto huyo ukiwa tayali umeshaliwa katika baadhi ya viungo.
Akiongea katika mkutano huo
mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ludewa Bw.Omary Kiowi alisema tukio
na kauli za mmiliki wa Mbwa hao wawili Bw.Bosco Lingalangala
hazivumiliki kwa wanaludewa kwani amekuwa akiwatishia wananchi kwa
kutumia bastola kila wakati hivyo kikao hicho kiliamuru mbwa hao wauawe
na mmiliki achukuliwe hatua za kisheria.
“Tokea nizaliwe zijawahi kuona
Mbwa akitafuna mtu, hii ni mara ya kwanza,hatuwezi kuvumilia na
ninachokiomba wananchi msifanye fujo naamini tukitoka hapa kwa
kushirikiana na ofisi ya mifugo pamoja na jeshi la Polisi tunakwenda
kumuua mbwa aliyebaki na tunamtaka Bw.Bosco atushtaki wananchi wote na
Serikali yetu kwa sababu anadhani yeye yuko juu ya sheria”,alisema
Bw.Kiowi.
Kufuatia kauli za vitisho wananchi
wakaomba kikao kiahirishwe na kuanza maandamano kuelekea katika nyamba
ya mmiliki wa mbwa hao ambako aliuawa marehemu Ibrahim na kuhakikisha
wananmuua mbwa aliyebaki kwa kupigwa risasi,kwa hasira walizo kuwa nazo
wananchi hao waliamua kuondoka na Mbwa hao wote wawili wakiwa wamekufa
na kupita nao mitaani huku wakiimba nyimbo mbalimbali.
Baada ya kuzunguka na mizoga ya
mbwa hao mitaani kwa muda mrefu hatimaye walielekea katika ofisi ya kata
na kuamua kuwachoma moto na kuwateketeza kabisa na kuendelea na kikao
ambacho kiliibua shangwe na vifijo baada ya mzee Laurance Mtweve
(Muhuchu) ambaye ni mzee mashuhuri kutoa kauli ya kuutaka uongozi wa
kijiji kumuandikia barua mkuu wa wilaya ya Ludewa ya kufukuza Bosco
kuishi eneo la Ikilu kutokana na vitisho vyake.
Mzee Muhuchu alisema kama uongozi wa wilaya utashindwa kufanya hivyo basi wazee wa wilaya ya Ludewa watamuandikia barua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuwa wamechoshwa na unyanyasaji wa Bw.Bosco hiyo hawamuhitaji wilayani hapa tena.
Alisema kwani imekuwa kawaida yake
kuwatisha wananchi kwa kutumia bastola hali inayowafanya wananchi
kuishi kwa kuhofia usalama wao kwani inaonekana yuko juu ya sheria
kutokana na kufanya matukio ya ajabu lakini wanaoshtaki hupuuzwa na
jeshi la polisi hapa Ludewa.
Aidha Diwani wa kata ya Ludewa
kupitia CCM mama Monica Mchilo aliwataka wananchi kupunguza jazba wakati
sheria inachukua mkondo wake ingawa awali alionesha kutoridhishwa na
kauli za mmiliki wa mbwa hao kuwa atawashtaki watakaohusika kuwaua.
Mama Mchilo alisema hakuna
aliyeridhishwa na kauli mbaya za Bosco lakini anaamini Serikali ni
sikivu itasikia kilio cha wananchi wa kata ya Ludewa kutokana na vitisho
vya mtu huyo ambaye hana hata chembe ya utu kwa kusema mbwa wasiuawe
bali atawalipa fidia wafiwa.
Aliwashukuru wananchi kwa kufanya
maandamano ya amani ambayo hayakuleta madhara kwa jamii lakini
yalifanikisha kuwaua mbwa ambao walikuwa ni tishio kwa jamii hasa kwa
wanafunzi wanaopita eneo hilo ambako aliwafugia mbwa hao.
0 Comments