Wema
Sepetu a.k.a Beautiful Onyinye amekula kiapo cha kumchukia dada wa
hiyari wa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’, Halima Kimwana
ambaye wamekuwa na bifu kwa kipindi kirefu huku sababu zikiwa
hazijulikani.
Akipiga
stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Wema alisema ugomvi wake na
Halima Kimwana hautaisha na siku zote atamuonyesha chuki za wazi sababu
hana upendo naye hata kidogo.
“Kusema
kweli yule dada namchukia mpaka basi, simpendi na sitompenda kamwe,
haitatokea hata siku moja kwenye maisha yangu nikapatana naye, yaani
suala la kupatana mimi na yeye halipo kabisa, hata yeye mwenyewe anajua
simpendi maana damu zetu zimekataana, siwezi hata kuonyesha upendo wa
maigizo kwake,” alisema Wema.
0 Comments