Advertisement

Responsive Advertisement

BEKI MPYA SIMBA SC AIDHINISHWA KUCHEZEA ZIMAMOTO LIGI KUU ZENJI

Shaffi Hassan ameidhinishwa kuchezea Zimamoto ya Zanzibar 
HATIMAE Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kimemuidhinisha rasmi mchezaji Shafii Hassan kukipiga katika timu ya soka ya Zimamoto, kwa msimu mpya wa ligi kuu Zanzibar inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 15.
Itakumbukwa kuwa mchezaji huyo pia amesajilia wa na Simba SC, huku Malindi nao wakija juu kwa kudai kuwa mchezaji huyo ni mali yao.
ZFA imefikia uamuzi huo baada ya kikaoa kilichofanyika katika ya viongozi wa Zimamoto, Malindi na ZFA, na kutafakari kwa kina juu ya sauala hilo, ambapo baada ya makubaliano yaliofikiwa mchezaji huyo aliidhinishwa kukipiga na Zimamoto.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina alikiri ZFA kumuidhinisha mchezaji huyo kuichezea Zimamoto, baada ya kikako kizito cha viongozi wa timu hizo kufikia muafaka  na hivi sasa ruhusa mchezaji huyo kukipiga na Zimamoto.
Kuhusu mchezaji kudaiwa kujiunga na Simba SC Ravia alisema kuwa mchezaji huyo hakusajiliwa na Simba, lakini alikwenda kwa ajili ya kufanya majaribio na sio kuwa alisajiliwa na timu hiyo.
Kwa upande wa Zimamoto kupitia katibu wake Ali Jongo alimeelezea furaha yake kwa ZFA baada ya kumuidhinisha kuchezea timu hiyo, ambayo ndiyo ilikuwa halali kuichezea baada ya kufuata taratibu zote zilizohitajika.
Katika hatua nyingine Jongo amewataka wachezaji wa kizanzibari kuwa makini na kutokubali kuhadaiwa hasa lwakati wa usajaili, kwani viongozi wa timu hasa kutoka Tanzania bara hujaribu kuwahadaa wachezaji.