Baiskeli ya walemavu iliyotolewa na msamaria
mwema wa Maryland Marekani, Joyce Rwehumbiza kwenda kwa
Bibi Scholastica Mhagama mkazi wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho
wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma.
MSAMARIA mwema mmoja ametoa baiskeli ya
walemavu kwa Bibi Scholastica Mhagama (76) mwenye ulemavu wa miguu
aliyeamua kijitengenea jeneza lake atakapozikwa baada ya kuishi maisha ya dhiki na kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi.
Bibi huyo mkazi wa Kijiji cha Lundusi, Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma anaishi peke yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.
Msamaria huyu kutoka Maryland, Marekani anaitwa Joyce Rwehumbiza na
aliguswa na stori iliyoandikwa na gazeti la Global Publishers ambapo
stori yake iko hapa: BIBI KIZEE AJIANDALIA JENEZA!
Joyce Rwehumbiza ameishatuma baiskeli hiyo na inafika Dar es Salaam leo Ahamisi ya Septamba 11, 2014.
0 Comments