Neema inazidi kumuangia Diamond
Platinumz na leo amepata habari njema baada ya kutajwa kuwania tuzo ya
MTV EMAs huku akipokea tuzo kutoka nchini Australia.
Diamond amewapa mashabiki wake habari njema za ushindi wa tuzo ya AAMA ya Australia kupitia tiketi ya collabo ya aliyopewa na Desert Eagle, wimbo unaoitwa ‘Everyday’.
“Ningependa niwajulishe kuwa kijana wenu nimepata tunzo nyingine toka Australia ya Collabo bora ya Mwaka toka kwenye tunzo za #AAMMA_Awards kupitia nyimbo niliyoshirikishwa na Desert Eagle iitwayo #EVERYDAY..... (jus wanted to inform you that, your favourite artist @Diamondplatnunz won another award from Australia on #AAMMA_Awards as best Collaboration song of the Year..).” Ameandika.
Wakati huo huo, mtoto wa Tandale ametajwa kuwa moja kati ya wasanii wanaowania MTV Europe Music Awards mwaka huu huku akichuana na wakali wengine kutoka Afrika akiwemo Davido, Toofan (Togo) na Goldfish (Afrika Kusini).
Msanii mwingine wa tano akisubiria kutajwa baada ya mashabiki kumpekeza kutoka kwenye kundi la wasanii sita ambao ni Anselmo Ralph, Gangs of Ballet, Mafikizolo, Sarkodie, Sauti Sol na Tiwa Savage.
Aidha, majina yote ya wasanii wanaowania tuzo hizo yatatajwa September 16 ambapo upigaji kura utaanza rasmi.
Hongera Diamond Platinumz, Tanzania inazidi kutajwa kwenye majukwaa ya kimataifa.