Baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kutokana na kusababisha madhara ya kiafya.
Asilimia
52 ya Watanzania wanawake kwa wanaume imedaiwa kuwa wanatumia vipodozi
ambavyo si salama kwa afya zao na ambavyo matumizi yake yamepigwa
marufuku nchini.
Afisa
kutoka asasi ya Envirocare Bi. Ephrasia Shayo amesema hayo wakati wa
kampeni ya kuzuia matumizi ya vipodozi hatari inayoendeshwa na asasi
hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA.
Bi.
Ephrasia ametaja baadhi ya madhara yanayotokana na matumizi ya vipodozi
hivyo kuwa ni saratani ya ngozi, kuzaa watoto wenye ulemavu wa akili,
kuharibika kwa mimba, maelezo ambayo yameungwa mkono na muelimishaji
umma wa TFDA Bw. James Ndege.
Kwa
mujibu wa Ndege, idadi kubwa ya vipodozi hivyo imeingia nchini kwa njia
za panya kutokana na hatua zinazochukuliwa na TFDA kudhibiti uingiaji
wa vipodozi hivyo katika mipaka.
Amesema
watu wengi wanakimbilia kunua vipodozi hivyo kutokana na kuuzwa kwa bei
nafuu ambayo kila mwananchi anaweza kuimudu pasipo kujali madhara
anayoweza kuyapata.
Muelimishaji
huyo kutoka TFDA amewataka wananchi kuchukua tahadhari zote kuepuka
matumizi ya vipodozi hatari, kama vile vyenye madini ya zebaki,
hydroquinone na nyinginezo ambazo zikiingia mwililini zinaleta madhara
makubwa kwenye viungo vya ndani ya mwili.
0 Comments