Mtangazajiwa
Kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM ya jijini
Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia
uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume.
Katika
mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva alisema
anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kumnyima uhuru wa kuongelea
suala lake na ‘zilipendwa’ wake huyo wakati kisheria yeye ni mke wake
hivyo anapaswa kuzungumzia kutengana kwao.
“Ninyi
mnayaongelea mambo ya Zitto na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi
nimeishi naye kama mke na mume nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini
kilisababisha penzi letu kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa
kutosha lakini wanaongeaongea tu,” alisema Diva.Akaongeza:
“Sasa
ninavyojua mimi kwa sheria za nchi, mwanamke na mwanaume wakiishi
pamoja kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na mume. Hawezi kuniacha
kirahisirahisi tu.”
Diva
alikwenda mbele zaidi kufuatia kauli ya Zitto aliyoitoa hivi karibuni
kupitia Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani na Runinga ya East
African Television ‘EATV’ na mtangazaji Salama Jabir.
Zitto aliulizwa ana uhusiano gani na Diva, naye akajibu ni mtu wanayefahamiana tu lakini si mpenzi wake.
Ilidaiwa
kwamba, majibu hayo ya Zitto kwa Salama ndiyo yaliyoibua hasira ya Diva
hadi kufikia hatua ya kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram, e-mail aliyodai aliwahi kutumiwa na Zitto siku za nyuma akimtaka asiwe anaweka wazi uhusiano wao kwa sababu atachafuka kisiasa.
E-mail ilisomeka hivi:
“Unanikosea
sana ujue unapoweka mambo yetu hadharani. Ninaonekana siwezi kuwa
kiongozi kwa sababu nashindwa ku-handle masuala yangu binafsi.
“Madhara uliyoyafanya ni makubwa sana. Wapinzani wangu wa kisiasa watayatumia sana dhidi yangu.
“Ungekuwa
unajua madhara yake usingethubutu kufanya ulivyofanya mara tatu sasa.
Sijui nia yako nini, ila ipo siku utajua umenikosea sanasana.”
Swali la mwandishi:
Je, Zitto akikubali kufuata huo utaratibu uwe mkewe utamuacha GK ambaye umekuwa ukimtangaza kuwa mpenzi wako?
Diva: Hilo nitakujibu baadaye.
Siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti uhusiano wa Diva na Zitto bila kuzama kwa undani.
Kufuatia
Diva kutupia madai hayo mtandaoni na kudai yeye ana hadhi ya mke kwa
Zitto na kauli ya Zitto kwenye runinga kwamba Diva si mpenzi wake,
baadhi ya watu waliozungumza na Amani walionesha kwenda kinyume na
mtangazaji huyo.
Wengi
walidai kwamba wana kumbukumbu zilizonyooka kwamba Diva amewahi
kujinadi kutoka na Mbongo Fleva, Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’.
“Sasa Diva anavyodai ni kama mke wa Zitto mbona anamtangaza mwanaume mwingine?” Alisema mkazi mmoja wa jiji aitwaye Yuda.
“Sasa Diva anavyodai ni kama mke wa Zitto mbona anamtangaza mwanaume mwingine?” Alisema mkazi mmoja wa jiji aitwaye Yuda.
Naye
Ismail Juma, mkazi wa Kigogo, Dar alisema aliwahi kusoma kwenye vyombo
vya habari kwamba Diva anapumzika na mwanamuziki kutoka Kenya, Jackson
Makini ‘Prezzo’ kiasi cha kumzalishia bifu na demu wa jamaa huyo, Huddah
Monroe.
“Diva awe na aibu basi, asikurupuke wakati yeye mwenyewe si msafi kivile,” alisema Ismail.
Kufuatia
madai hayo, kwa muda wa siku saba, Amani limekuwa likimsaka Zitto kwa
njia ya simu lakini bila mafanikio.Watu wa karibu naye walipoulizwa
alipo, walisema wanachojua ana shughuli zake nchini Zambia.
0 Comments