Mchekeshaji
maarufu hapa Tzee ambaye anamiondoko ya kimasai, Gillady Severina aka
Masai Nyotambofu, ameteka sana soko la filamu hapa Bongo kwa upande wa
Comedy kwa kufanya filamu kibao kama ‘Vyumba Vimejaa’, ‘Inye
Ndembendembe’, ‘Pedeshe’ nk.
Kwa chanzo chetu cha kuaminika kimebaini uhusiano uliopo baina ya Masai Nyotambofu na Salma Jab aka Nisha anayetamba sokoni na muvi ya ‘Zena Na Betina’, ‘Jike Dume’ nk, mara baada ya kuunasa Comment yake Instagram aliyopost kidume mwenye mbwembwe za kimasai. BK lilijaribu kumuuliza Nyotambofu ambye alijibu hivi,
“No jamani mimi sina mahusiano yeyote na Nisha but mimi siku ile nilipost tu kuwataarifu watu juu ya kutoka kwa muvi yake Nisha iliyofahamika kwa jina ‘Zena Na Betina’ basi najua Nisha alitoa Coment hiyo kwasababu aliona kuwa mimi jinsi gani napenda mafanikio yake.” alisema Masai Nyotambovu.